RealBiz ni kampuni inayojihusisha na uuzaji wa viwanja katika mikoa ya Dar es Salaam na Tanga. RealBiz inapenda kuwatangazia vijana wa Kitanzania fursa ya ajira katika shirika letu.
RealBiz inahitaji vijana wenye uzoefu, ambao wana uwezo wa kufanya vyema katika nyanja zifuatazo kwa kuzingatia misingi yetu ya maadili katika utendaji wetu wa kazi ambao ni uwajibikaji, uadilifu, umiliki na mawazo chanya juu ya kampuni.
NAFASI ZILIZOPO
1. Afisa Mauzo na Masoko
NAFASI ZILIZOPO: 4
Aina ya Ajira: Ajira ya kudumu/Ajira ya Muda mfupi
MAJUKUMU
- Awe na uwezo kuleta wateja, kuandaa vikao vya mauzo na kufikia malengo ya mauzo.
- Awe na uwezo wa kufanikisha mazungumzo ya kibiashara
2. Muendeshaji wa ofisi
Nafasi zilizopo: 1
Aina ya Ajira: Ajira ya kudumu
MAJUKUMU
- Kuwajibika kwa usimamizi wa ofisi na shughuli za dawati. Kuwa na ujuzi wa HR ni faida ya nyongeza.
MAHITAJI:
Waombaji wote lazima wawe raia wa Tanzania wenye angalau astashahada ya masoko, rasilimali watu, tecknolojua ya mawasiliano, uhasibu, au fani zinazohusiana.
Kampuni itawasiliana na watakaovuka mchujo wa kwanza.
Njia ya Maombi
Mwombaji lazima ajaze sehemu zote zinazohitajika na kuwasilisha viambatisho vyote.
Maombi lazima yafanywe mkondoni kupitia portal yetu ya Kazi kwa kutumia kiunga kilicho hapa chini:
Tuma maombi hapa:
Waweza pia kutuma maombi yako kupitia realbizcompany@gmail.com au +255 754 710 678
Tarehe ya mwisho: Mfumo utaacha kupokea maombi tarehe 20/10/2023 saa 01:00 jioni.